18 Februari 2015 - 19:37
Umoja wa Ulaya wawashutumu waasi Ukraine

Mkuu wa sera ya nje ya Umoja wa Ulaya bibi Federica Mogherini amewalaumu waasi wanaoelemea upande wa Urusi kuvunja makubaliano ya kuweka chini silaha Mashariki ya Ukraine kwa kuuzingira mji muhimu wa Debaltzewe,akisema Umoja wa Ulaya uko tayari kuchukua hatua zinazohitajika ikiwa mapigano yataendelea."

Mkuu wa sera ya nje ya Umoja wa Ulaya bibi Federica Mogherini amewalaumu waasi wanaoelemea upande wa Urusi kuvunja makubaliano ya kuweka chini silaha Mashariki ya Ukraine kwa kuuzingira mji muhimu wa Debaltzewe,akisema Umoja wa Ulaya uko tayari kuchukua hatua zinazohitajika ikiwa mapigano yataendelea."Visa vya waasi katika mji unaozingirwa wa Debaltzewe ni uvunjwaji bayana wa makubaliano ya kuweka chini silaha" amesema bibi Mogherini katika taarifa yake.Amewataka wanamgambo hao wanaopigania kujitenga eneo la mashariki la Ukraine wasitishe harakati zao za kijeshi.Amewatolea wito waasi na Urusi watekeleze kikamilifu makubaliano ya Minsk kuambatana na azimio lililopitishwa jana na baraza la usalama la Umoa wa mataifa.Wakati huo huo serikali ya Ujerumani mjini Berlin imelaani mashambulio ya waasi Mashariki ya Ukraine na kusema "yanavuruga matumaini ya kupatikana amani. "Ujerumani inalaani kwa nguvu opereshini za kijeshi za waasi huko Debaltzeve" msemaji wa kansela Angela Merkel,Steffen Seibert amesema na kuongeza tunanukuu:"ni uvunjwaji mkubnwa wa makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa Minsk.

Wakati hayo yanaendelea Rais Petro Poroshenko wa Ukraine amethibitisha ripoti za kurejea nyuma wanajeshi wa nchi yake toka mji unaozingirwa wa Debalzeve.

Rais Porochenko amesema  mjini Kiev kwamba hadi wakati huu,wanajeshi wanne kati ya watano wameshauhama mji huo muhimu.Waasi wamekuwa wakidhibiti sehemu kubwa ya mji huo muhimu kwa safari za reli tangu jana.Rais Poroshenko alifunga safari hadi katika mji huo katika eneo la mzozo la Donbass.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi,Serguei Lavrow amesema yakitengwa matukio ya Debalzewe,makubaliano ya kuweka chini silaha yanaheshimiwa katika sehemu zote nyengine za mapigano.